Staili za maisha/mitindo

Jinsi mwanaume mrefu avae ili apendeze:

Mwanaume anahitaji kutokuwa nje ya mitindo au kutoenda na wakati linapookuja swala la mavazi hasa kwa wale walio warefu. Mwili wa mwanaume mrefu ni tofauti kidogo katika muundo. Hivyo hawana fursa ya kuvaa nguo yoyote.


Wabunifu wa mavazi/mitindo ya wanaume mara nyingi wamekuwa wakitengeneza na kubuni nguo kulingana na mwili ulivojengeka, kwa mwanaume mrefu ni vigumu kupata nguo ambayo itamtosha vizuri.
Sasa nikupe dondoo kidogo za kuzingatia wakati wa kuchagua nguo ya kuvaa;
Kama ni mwembamba na mrefu, basi epuka nguo ya kubana, chagua nguo ya kitambaa laini, pia epuka nguo yenye mistari wima kwani itakufanya uonekane kuwa mwembamba na mrefu zaidi. Unatakiwa kuvaa shati lenye nakshi mbali mbali.
Hakikisha unavalia suruali yako juu kidogo au chini kidogo ya kiuno, usije kamwe ukavaa juu ya tumbo.

Pia vaa suruali ndefu zaidi ya urefu wako wa kawaida, hakikisha suruali yako isiwe fupi.
Epuka kuvaa nguo zenye rangi moja kwanni zitakufanya uonekane mrefu zaidi. Kama unataka kuvaa fulana, basi ile yenye kola itafaa zaidi. Epuka kuvaa nguo ya kubana(modo) hususani jeans, chagua nguo itakayokupa uhuru wakati wa kutembea.