BOOX |
1. Jina lako la kisanii?
Jina ni Boox.
2. Ni muda gani umekua katika music game?
Niko kwenye game miaka 12 sasa.
3. Nini kilikupelekea kufanya mziki? au ulijuaje unakipaji cha music?
Bana nilijitambua kwanza me ni HipHop, na kuna watu wakanifanya niwe more deep, kama Das efx, Onyx, na wengine.
BOOX |
Mziki wangu au KCK, inacheza na halisia ya kwenye jamii, in general life and everything inayotuzunguka, Reality!
5. Ni kitu gani hukupelekea kuandika nyimbo?
Ni feelings nilizonazo mda huo, au kitu nilicho kiona na ikanipa mzuka wa kuandikia nyimbo.
6. Unamalengo gani miaka mitano ijayo na muziki wako?
miaka mitano ijayo nataka niwe na hip hop music foundation, kuhakikisha Hiphop inadumu forever, na hata nikifa nimeacha kitu muhimu sana, ya kuendeleza harakat!
7. Kupitia internet mtu anawezaje kupata muziki wako?
Napatikana instagram @ booxkck, facebook @ booxkck, Twitter @ booxkck, tunayo page just write Kck supremacy, like it u will get more from me and ma blood Spac Dawg. Pia mziki wangu unapatikana mkito.com
KCK SUPREMACY |
Mkali huyu pia alizungumzia nyimbo yao iliyotoka hivi karibuni inayotambulika kwa jina la Fekeche fekeche, alisema katika nyimbo hiyo iliyoandikwa katika lugha ya kufurahisha verse yake aliongelea maisha na mwenzake Spac Dawg aliongelea mapenzi yote yakiwa sehemu ya maisha yanayotuzunguka katika jamii.
Pia alisema t-shirt tayari zipo mtaani na video ya wimbo huo inatarajiwa kutoka mwishoni mwa mwezi huu mashabiki wao wakae tayari kuwapa support.